WIN $100 GIFT VOUCHERS: PROMOTIONS

Close Notification

Your cart does not contain any items

Noah Henry

Hadithi ya Upinde wa Mvua

Deana Sobel Lederman

$18.95

Paperback

Not in-store but you can order this
How long will it take?

QTY:

Swahili
Calec
15 October 2020
Kama siku yoyote nyingine, Noah Henry anajitayarisha kwenda shuleni-lakini, wazazi wake wanamwambia kwamba shule yake imefungwa. Zaidi ya hilo, bustani ya wanyama pia imefungwa na hataweza kucheza na rafiki zake wanaoishi mle. Mambo hayabadiliki hata wakati Noah na kaka yake mdogo wananawisha mikono yao kama walivyoambiwa na walimu wao. Lakini, wakati Noah na familia yake wanapoondoka kwenda matembezini, anagundua ya kwamba rafiki zake walikuwa wamechora pinde za mvua na kuziweka kwenye madirisha yao, na anatambua ya kwamba rafiki zake pia hawana hakika kuhusu siku zijazo, na ya kwamba siku moja yeye na rafiki zake watacheza pamoja tena.
By:  
Imprint:   Calec
Edition:   Swahili ed.
Dimensions:   Height: 216mm,  Width: 216mm,  Spine: 2mm
Weight:   91g
ISBN:   9781636070223
ISBN 10:   1636070221
Series:   Rainbows, Masks, and Ice Cream
Pages:   30
Publication Date:  
Recommended Age:   From 1 to 10 years
Audience:   Children/juvenile ,  English as a second language
Format:   Paperback
Publisher's Status:   Active

Deana Sobel Lederman ni mwandishi na mchoraji. Bibi yake alikuwa mchoraji ambaye alisomea kwenye chuo kiitwacho The Art Students League of New York. Alimfundisha Deana kuhusu uchoraji wakati Deana alikuwa mchanga sana, na mamake Deana pia alimhimiza kuchora kutoka wakati Deana alikuwa mchanga. Deana alichora kitabu chake cha kwanza cha ucheshi kinachoitwa The Wacky Couples wakati alikuwa na miaka minane, na baadaye alikuwa mchoraji mkuu wa gazeti la wanafunzi wa UC Berkeley na msanii aliyechapishwa. Baadaye, alisomea kuhusu sheria ya hakimiliki kwenye chuo kikuu cha sheria. Ameishi New York City; Berkeley, California; London, England; na Cambridge, Massachusetts. Deana alikulia katika mji wa San Diego, California, na hapo ndipo anapoishi pamoja na mume wake na watoto wake wawili.

Reviews for Noah Henry: Hadithi ya Upinde wa Mvua

"Michoro katika kitabu hiki ni ya kupendeza sana. - Sam Gross, Msanii wa New Yorker Deana Sobel Lederman ana zawadi ya kuandika kwa watoto na uwazi na fadhili na ucheshi. Michoro yake inakamilisha maandishi yake na urahisi wa kuelewa wake inatukumbusha kazi ya Jean de Brunhoff. - Victoria Roberts, Msanii wa New Yorker Iliotungwa wakati wa ""Mgogoro Mkubwa,"" Upinde wa Mvua, Barakoa, na Aiskrimu zilituletea furaha na njia nzuri ya kuzugumza na watoto wetu kuhusu virusi vya Corona. Kuweza kusoma hivi vitabu kwa lugha zetu pia ilimaanisha kwamba vilikuja karibu na mioyo yetu. - Dr. Fabrice Jaumont, mwandishi na mwalimu. Sikuweza kushiriki Noah Henry na waalimu wangu na marafi ki zangu kwa muda ambao ningependa. Deana alichukua hali zetu za sasa na kuzionyesha kupitia macho ya mtoto kwa njia ambayo singeweza kufanya kamwe kama mama au mwalimu. - Alexa Ingram Msimamizi wa wilaya ya shule & Mama Bado kuna cheche za mwangaza katika nyakati za giza sana. Nilipata hadithi inayohimiza ya Noah Henry na upendo wake wa pinde za mvua, ilioandikwa na Deana Sobel Lederman, kwenye mitandao ya kijamii. Michoro katika kitabu hiki zilinivuta kwenye hadithi ya hamu ya kijana mmoja kuungana na wanafunzi wenzake wakati wa janga hii. Hadithi hii ya kupendeza itawafurahisha wasomaji na kuwapa ujumbe wa matumaini. - Robin Cogan Muugizi wa shule"


See Also